Shirika la Habari la Kimatifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majalis za Muharram zinaendelea katika mimbari mbalimbali za Imam Hussein (as) katika Jiji la Arusha. Waumini wengi wanajitokeza kutoka maeneo mbalimbali na kushiriki katika Vikao vya Kielimu kuhusiana na Mapinduzi ya Kiislamu ya Imam Hussein (as) katika Ardhi ya Karbala. Katika picha ni Majlisi ya Darsa kuhusiana na Mapinduzi ya Karbala, waumini wa Kiislamu wakiwa katika mkao wa kusikiliza historia ya Mapinduzi ya Haki ya Imam Hussein (as) dhidi ya Batili ya Yazid bin Muawiya(la), ikiwa ni mada iliyotolewa na Samahat Sheikh Bashir Bar'wan katika Husseiniyya ya Ahlul-Bayt (as) Jijini Arusha - Tanzania.

1 Julai 2025 - 18:22

Mimbari ya Imam Hussein (as), Arusha- Tanzania | "Map[induzi ya Haki ya Imam Hussein (as) dhidi ya Batili ya Muovu Yazid bin Muawiya"

Your Comment

You are replying to: .
captcha